Polisi waanza uchunguzi maafa Seoul

0
190

Polisi nchini Korea Kusini wameanza uchunguzi, ili kubaini chanzo cha tukio la kukanyagana na kusababisha vifo vya watu 153.

Watu hao wamekanyagana na kufariki dunia wakati wa tamasha la Halloween katika mji mkuu wa Seoul.

Tukio hilo limetokea wakati umati mkubwa wa vijana waliokuwa wakishiriki kwenye tamasha hilo katika eneo linaloelezwa kuwa ni dogo kubanana na hatimaye kuanza kukanyagana.

Watu wengine 150 wamejeruhiwa katika tukio linalotajwa kuwa ni baya zaidi kuwahi kutokea Korea Kusini katika miaka ya hivi karibuni.

tamasha la Halloween linaadhimishwa katika maeneo mbalimbali duniani Oktoba 31 ya kila mwaka, kwa lengo la kuwakumbuka wafu wote duniani.