Rais atoa pole, vifo vya watu 149 Seoul

0
249

Rais Samia Suluhu Hassan amemtumia salamu za pole Rais wa Korea Kusini, kufuatia vifo vya watu 149 vilivyotokea baada ya kukanyagana wakati wa tamasha la Halloween lililofanyika katika mji wa Seoul.

Katika salamu zake alizozituma kupitia ukurasa wake wa twitter, Rais Samia amesema Tanzania inaungana na wananchi wote wa Korea Kusini katika kuomboleza msiba huo mzito na kuwaombea majeruhi wapone haraka.