Robertson aitahadharisha Man U

0
588

Mlinzi wa timu ya Liverpool ya nchini England, -Andrew Robertson ameitahadharisha Manchester United kuwa makini na safu ya ushambuliaji ya klabu yake,  kuelekea mchezo wa ligi Kuu ya nchi hiyo ambao timu hizo zitapepetana siku ya Jumapili.

Nyota huyo amesema wanatambua kuwa Manchester United ina wachezaji wanaoweza kuwaletea madhara,  lakini nao safu yao ya ushambuliaji ipo imara sana na kiu yao ni kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England.

Robertson ameyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa pambano la ligi ya mabingwa Barani Ulaya dhidi ya timu ya Bayern Munich ya Ujerumani ambapo mchezo huo ulimalizika kwa suluhu.

Kwa upande wake kocha wa Liverpool, -Jurgen Klopp amekishushia lawama kikosi chake kwa kushindwa kutengeneza pasi za kufunga mabao kwa washambuliaji wake, jambo ambalo anasema limesababisha kikosi chake kupata matokeo hayo ya suluhu.

Hata hivyo Klopp amesema kuwa matokeo hayo ni mazuri kwao,  kwani wataingia kwenye mchezo wa marudiano nchini Ujerumani wakiwa bila deni.