Ni TEMS

0
1544

Hadharani kupitia ukurasa wake wa Instagram Temilade Openiyi maarufu kwa jina la Tems (@temsbaby) msanii kutoka nchini Nigeria, amethibitisha kushiriki katika kuandika ngoma mpya ya Rihanna “Lift Me Up” iliyoachiwa mwaka huu.

Wimbo huo ni Soundtrack ya filamu ya “Black Panther 2: Wakanda Forever” .

Inasemekana kuwa wimbo huo wa “Lift Me Up” ni wa kumuenzi marehemu Chadwick Boseman, nguli ambaye aliigiza filamu ya Black Panther, ambayo ni ya kwanza kabla ya kufariki dunia kwa saratani mwaka 2020.

Katika kuandika wimbo huo wa “Lift Me Up” Tems ameshirikiana na Ludwig Göransson (mtayarishaji na mtunzi aliyeshinda tuzo za Oscar), Ryan Coogler (aliyeongoza sinema zote mbili za Black Panther) na Rihanna mwenyewe.

Rihanna amemshukuru Tems hadharani kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa uandishi wake katika wimbo wake mpya “Lift Me Up”.

Tems ni miongoni mwa wasanii wakubwa wa pop walioibuka barani Afrika mwaka 2020, na ni mshindi wa tuzo ya BET 2022.