Dkt. Rioba ahimiza matumizi ya mitandao ya kijamii katika habari

0
375

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba akiwasilisha mada katika mkutano wa vyombo vya habari vya utangazaji na mabadiliko ya kidigitali Kigali nchini Rwanda.

Katika mkutano huo Dkt. Rioba ametoa wito kwa vyombo vya habari vya umma kwenda na kasi ya mabadiliko ya kiteknolojia ikiwemo kiweka nguvu kwenye mitandao ya kijamii ambapo ndipo watazamaji na wasikilizaji walipohamia.

Pia amebainisha kuwa katika mwaka huu wa fedha, TBC imetenga bajeti maalum kwa ajili ya kufanya utafiti wa kufahamu aina ya maudhui ambayo watazamaji na wasikilizaji wa TBC wanayataka.