Iringa watakiwa kudhibiti ulevi kwa wajawazito

0
312

Mkuu wa mkoa wa Iringa, Halima Dendego amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri katika mkoa huo kusimamia sheria ndogo za kudhibiti ulevi uliokithiri kwa wananchi hususani akina mama wajawazito ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na lishe duni kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano mkoani humo.

Akizungumza kwenye kikao cha utiaji saini wa mkataba wa lishe na wakurugenzi wa halmashauri, Dendego amesema utafiti umegundua kuwa ulevi wa kupindukia ni chanzo kimojawapo cha lishe duni kwa watoto kwa kuwa wazazi hawaangalii watoto wao.

Wakurugenzi wa halmasahuri wamesaini mikataba ya lishe ya miaka nane kwa ajili ya utekelezaji kwenye halmashauri zao huku kipaumbele ni chakula mashuleni na kutengwa kwa bajeti ya lishe kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.