Kandege aendelea na ziara Rukwa

0
726

Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Manispaa nchini wametakiwa  kuboresha miundombinu ya ofisi za walimu ili kuwawekea mazingira mazuri ya kutayarisha masomo kwa ajili ya wanafunzi na maeneo mazuri ya kupumzika.

Wito huo umetolewa mkoani Rukwa na Naibu Waziri wa Nchi,  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – Tamisemi, -Japhet Kandege wakati wa kukabidhi samani kwa baadhi ya wakuu wa shule za sekondari na msingi katika halmashauri ya wilaya ya Kalambo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo,-Efreim Moses amesema kuwa jamii inatakiwa kushirikiana na serikali katika kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia.

Naibu Waziri huyo wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, – Japhet Kandege anaendelea na ziara yake ya kikazi wilayani Kalambo  kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.