Hakuna kurithi silaha

0
217

Mkuu wa kitengo cha Usimamizi, Udhibiti wa Usajili Silaha na Leseni kutoka jeshi la polisi nchini Reinada Millanzi amesisitiza kuwa, hakuna urithi wa silaha kwa sababu mtu anapoomba leseni ya umiliki wa silaha lazima aseme sialha ni ya nini au anaitaka kwa sababu gani.

Amesema hata mmiliki akifariki dunia silaha hiyo si ya kurithi.

“Mara baada baba au ndugu anapofariki ile silaha inanyanyuliwa ipelekwe kwenye kituo cha polisi ikahifadhiwe wakati taratibu za mirathi zikiendelea , hizi ni kwa ajili ya zile silaha halali, sio haramu na si gobore.”  amesema Millanzi

Mkuu huyo wa kitengo cha Usimamizi, Udhibiti wa Usajili Silaha na Leseni kutoka jeshi la polisi nchini ameyasema hayo katika mahojiano kwenye kipindi cha Jambo Tanzania ambapo hasa amezungumzia  zoezi la kusalimisha silaha kwa hiari.

https://youtu.be/ca-8FXSuZ5g

Pia amebainisha kuwa silaha ambazo zimeingia nchini kinyume na taratibu ni haramu na hata kama mtu amenunua na kumiliki ajue ni haramu.