Rais amteua Kaganda Jeshi la Polisi

0
376

Rais Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Suzan Kaganda kuwa Kamishna wa Polisi.

Baada ya kumpandisha cheo, Rais Samia amemteua Kamishna Kaganda kuwa Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu wa Jeshi la Polisi.

Kamishna Kaganda anachukua nafasi ya Benedict Wakulyamba ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Uteuzi huo unaanza mara moja.