Johnson ajiondoa kinyang’anyiro cha uwaziri mkuu

0
297

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Boris Johnson amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha uwaziri mkuu wa nchi hiyo.

Hatua ya Johson kujiondoa katika kinyanganyiro hicho inampa nafasi kubwa Rishi Sunak kuchaguliwa kushika wadhifa huo ikiwa imepita takribani miezi miwili baada ya kushindwa katika kinyang’anyiro kingine cha kumpata Waziri Mkuu wa Uingereza.

Kinyang’anyiro cha kumpata Waziri Mkuu mpya wa Uingereza kinafuatia kujiuzulu kwa Liz Truss, ambaye amehudumu katika wadhifa huo kwa siku 45 pekee.

Upinzani mkali katika kinyang’anyiro hicho cha Uwaziri Mkuu nchini Uingereza kilionekana kati ya Boris Johnson na Rishi Sunak.

Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo atatakiwa kuungwa mkono na wabunge wasiopungua mia moja wa chama cha Conservative kwa njia ya kura, shughuli ambayo imepangwa kufanyika baadae hii leo.

Habari zaidi kutoka nchini Uingereza zinaeleza kuwa, mpaka sasa Rishi Sunak anaungwa mkono na wabunge takribani 150.