‘Bon Vol’ Felix Tshisekedi

0
174

Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ( DRC), ameondoka nchini hii leo baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere mkoani Dar es Salaam, Rais Tshisekedi ameagwa na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan.

Akiwa hapa nchini, hapo jana Rais Tshisekedi pamoja na mambo mengine alipokelewa na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan na kuwa na mazungumzo ya faragha Ikulu, Dar es Salaam.

Viongozi hao pia walishuhudia utiaji saini wa mikataba inayohusu ushirikiano wa mawasiliano kati ya Tanzania na DRC.

Hiyo ilikuwa ni ziara ya kwanza ya Rais
Tshisekedi nchini Tanzania tangu serikali ya awamu ya sita ilipoingia madarakani, na ni ziara yake ya pili akiwa Rais wa DRC.