Rais Felix Tshisekedi kuwasili Dar es Salaam leo

0
241

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi Tshilombo anatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam leo kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Rais Tshisekedi atapokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Ujio wake ni wa kwanza katika uongozi wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Matangazo ya mapokezi ya ujio huo yatakujia mbashara kupitia TBC1, TBC Taifa na mitandao yetu ya kijamii kwa anwani ya TBCOnline.

tbconline #tbcupdates #congo #raiscongo