Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi ambapo amemteua Dkt. Florens Turuka, Katibu Mkuu mstaafu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).
Pia amewateua maafisa watano kuwa wajumbe wa Bodi ya DART ambao ni Zainab Msimbe (Mhasibu Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali), Mhandisi Johansen Kahatano (Mkurugenzi wa Barabara, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini –
LATRA), Aron Kisaka (Mkurugenzi wa Huduma za Usafirishaji, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi), Benjamini Dotto (Mkurugenzi wa Miundombinu, Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) na Mwantumu Salim (Katibu EPZA).
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Beng’i Mazana Issa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa.
Beng’i ni Katibu Mtendaji, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).
Wengine walioteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni maafisa watano kuwa wajumbe wa bodi ya mikopo ya Serikali za Mitaa.
Wajumbe hao ni Hemed Mpili (Afisa Ugavi Mwandamizi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI), Profesa Provident Dimoso (Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Dodoma), Said Panga (Mkuu wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimali Watu, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Dodoma), Joseph Chilambo ( Meneja Uendeshaji Biashara, Benki ya Maendeleo ya TIB na John Cheyo (Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Ofisi ya Rais).
Uteuzi huo umeanza tarehe 20 mwezi huu.
Wengine walioteuliwa na Rais Samia ni Profesa Tumaini Nagu ambaye anakuwa Mganga Mkuu wa Serikali.
Kabla ya uteuzi huo Profesa Nagu alikuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Tiba, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Profesa Nagu anachukua nafasi ya Dkt. Aifello Sichalwe ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Uteuzi wa Profesa Nagu umeanza tarehe 19 mwezi huu.
Deusdedit Bwoyo yeye ameteuliwa na Rais kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, wizara ya Maliasili na Utalii.
Kabla ya uteuzi huo Bwoyo alikuwa Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Misitu na Nyuki.
Uteuzi wa Bwoyo umeanza tarehe 20 mwezi huu.
Mwingine aliyeteuliwa ni James Sando kuwa Katibu Mtendaji wa Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma (PPAA).
Sando alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Fedha Kampuni ya Crown Accounting and Consulting Firm, Dar es Salaam.
Uteuzi wa Sando umeanza tarehe 20 mwezi huu.