Ng’anzi, mkuu mpya wa Kikosi cha Usalama Barabarani

0
299

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Camillus Wambura amefanya mabadiliko madogo ndani ya jeshi hilo, ambapo amewahamisha baadhi ya makamanda wa polisi kutoka nafasi zao na kuwapangia sehemu nyingine.

Katika mabadiliko hayo madogo Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng’anzi amehamishwa na kuwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania.

Ng’anzi anachukua nafasi ya Wilbroad Mtafungwa aliyekuwa Mkuu wa kikosi hicho ambaye sasa amehamishwa na kuwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza.