Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu amewaomba wasanii nchini kufanya kazi zao kwa weledi ili waendelee kuwa kioo cha jamii.
Wema ameyasema hayo jijini Dar es salaam baada ya kuondolewa adhabu yake ya kutofanya kazi za sanaa, adhabu iliyotolewa na Bodi ya Filamu nchini.
Akizungumza na Waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu nchini Joyce Fisoo amesema kuwa bodi hiyo imeamua kumfungulia Wema ili aweze kuendelea na kazi yake ya uigizaji wa filamu baada ya kutimiza masharti aliyopewa.
Wema alifungiwa na Bodi ya Filamu Nchini kujihusisha na kazi za Filamu kwa kipindi kisichojulikana, kwa kosa la kusambaza video zisizokuwa na maadili katika jamii.