Mbeya City yaipopoa Polisi Tanzania 3-1

0
722

Mbeya City imefanikiwa kuutumia vizuri uwanja wa nyumbani wa Sokoine mkoani humo na kuondoka na alama tatu baada ya kuiadhibu Polisi Tanzania FC kwa magoli 3-1.

Polisi Tanzania ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli kabla ya Mbeya City kusawazisha na kufunga magoli ya ushindi.

Kwa ushindi huo vijana wa Mbeya wanapanda hadi nafasi ya 6 wakiwa na alama 9 baada ya kushuka dimbani mara 7, huku Polisi Tanzania ikiburuza mkia katika nafasi ya 16 ikiwa na alama 2 baada ya kucheza michezo 7.

Mara ya mwisho timu hizi zilikutana Mei 15, 2022 ambapo zilitoka suluhu.