Kasoro tisa ambazo mwenge umezibaini katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo

0
877

  1. Matumizi ya fedha nyingi za umma yasiyoendana na thamani halisi ya mradi husika ‘no value for money’.
  2. Miradi kutekelezwa kinyume na mikataba ya kisheria iliyokubaliwa na makadirio yaliyopitishwa na wataalamu.
  3. Kufanya malipo ya wakandarasi bila kuwepo kwa hati za kuthibitisha ukamilishwaji wa kazi inayolipwa.
  4. Kutozingatiwa taratibu za malipo ya fedha za umma na taratibu za manunuzi.
  5. Ukwepaji kodi katika miradi mingi.
  6. Matumizi ya vifaa duni vya ujenzi na ukiukwaji wa kanuni za ujenzi zinazokubalika kihandisi.
  7. Wakandarasi wanaotekeleza miradi hawasimamiwi kikamilifu na wahandisi katika halmashauri.
  8. Watumishi kubebeshwa majukumu mazito ambayo mengine hawana weledi nayo.
  9. Upotevu na ufichaji wa nyaraka za malipo katika miradi, hali inayoashiria malipo hewa na matumizi mabaya ya fedha.

https://www.instagram.com/p/CjsUdE5oBSE/

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka huu Sahili Geraruma ameyasema hayo mkoani Kagera wakati wa kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan.