Saudia na Pakistani zasaini mikataba ya uwekezaji

0
687

Saudi Arabia na Pakistani zimesaini mikataba ya uwekezaji yenye thamani ya Dola Bilioni 20 za Kimarekani.

Mikataba hiyo imesainiwa wakati wa ziara ya Mwanamfalme wa Saudia Arabia, – Mohammed Bin Salman nchini Pakistani.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa mikataba hiyo, Waziri Mkuu wa Pakistani, -Imran Khan ameishukuru Saudi Arabia ambayo ni mshirika wake wa muda mrefu na kuongeza kuwa mikataba hiyo itaisaidia Pakistani kuokoa uchumi wake.

Mwanamfalme huyo wa Saudia Arabia anaendelea na ziara yake katika nchi Tatu za Bara la Asia, na akikamilisha ziara yake nchini Pakistani ataelekea nchini India ambapo atakutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Narendra Modi pamoja na Waziri wa Petroli na Gesi Asilia wa nchi hiyo Dharmendra Pradhan.

Nchi nyingine ambayo Salman ataitembelea ni China, ambapo lengo la ziara hiyo katika nchi hizo Tatu ni kukuza uhusiano wa kibiashara.