Misa ya kumuombea Baba wa Taifa

0
244

Leo ni kumbukizi ya miaka 23 tangu kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarange Nyerere aliyefariki dunia Oktoba 14 mwaka 1999 huko London nchini Uingereza.

Katika kukumbuka ya siku hiyo Rais
Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango wameshiriki Misa ya kumuombea Hayati Nyerere iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Katoliki la Bukoba mkoani Kagera.

Shughuli nyingine inayofanyika hii leo pamoja na kumbukizi hiyo ya kifo cha Baba wa Taifa ni kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru.