Mwanamuziki mashuhuri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) Verckys Kiamuangana Mateta amefariki dunia huko Kinshasa akiwa na umri wa miaka 78.
Verckys amefariki dunia baada kupatwa na maradhi ya kiharusi miezi kadhaa iliyopita.
Barani Afrika Verckys na Manu Dibango ndio walikuwa na uchawi wa kupuliza Saxaphon, na alikuwa ni mwanamuziki na mfanyabiashara mkubwa.
Alimiliki bendi kadhaa zilizotamba katika miaka ya 70 na 80 kama vile Ochestra Veve, Lipua Lipua na Kiam.
Pia alimiliki studio ya kurekodi iliyokuwa ikiitwa Edition Veve ambayo bendi nyingi maarufu enzi hizo zikiwemo Lipua Lipua, Les Kamale, Shama Shama, Bella Bella, Kiam, Zaiko Langa Langa zilirekodi nyimbo zao kwake.
Verckys Kiamuangana Mateta ameacha watoto 32, huku wawili ambao ni Ancy na Daniel wakifuata nyayo zake katika muziki.