Miaka 23 tangu Kifo cha Baba wa Taifa (Nyerere Day)

0
187

Leo ni kumbukizi ya miaka 23 tangu kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyefariki dunia Oktoba 14 mwaka 1999 huko London nchini Uingereza.

Kumbukizi hiyo inafanyika pamoja na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na kilele cha wiki ya Vijana Kitaifa.

Shughuli zote hizo zinafanyika katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera ambapo mgeni rasmi ni Rais Samia Suluhu Hassan.