Rais atoa pole kifo cha Mbunge

0
274

Rais Samia Suluhu Hassan amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson kufuatia kifo cha Mbunge wa jimbo la Amani mkoa wa Mjini Magharibi Mussa Hassan Mussa kilichotokea Zanzibar hii leo.

Katika salamu zake Rais Samia amesema amepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mussa Hassan Mussa ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika utumishi wa umma.

Rais Samia amemuomba Spika wa Bunge kufikisha salamu zake za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na watu wote walioguswa na msiba huo.