Mbunge wa jimbo la Amani afariki dunia

0
188

Mbunge wa jimbo la Amani lililopo Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mussa Hassan Mussa, amefariki dunia hii leo huko Zanzibar.

Taarifa ya kifo cha Mbunge Mussa Hassan Mussa imetolewa na Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, ambaye ametoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wabunge pamoja na wananchi wa jimbo la Amani kufuatia msiba huo.