Rais Samia amwaga bilioni 3.3 za maendeleo Makete

0
193

Wilaya ya Makete mkoani Njombe imepokea shilingi bilioni 3.312 ambazo ni
fedha za maendeleo awamu ya kwanza.

Fedha hizo ni kutoka serikali inayoongozwa na ya Rais Samia Suluhu Hassan na zimeelekezwa kwenye miradi ya maendeleo wilayani humo.

Akizungumza katika kikao kazi cha watendaji na wataalamu wa wilaya ya Makete, Mbunge wa jimbo hilo Festo Sanga ametaka fedha hizo zitumike kama ilivyokusudiwa.

” Tumepokea fedha nyingi za maendeleo kutoka serikalini, haijawahi kutokea na hii ni awamu ya kwanza. Fedha hizi zinakwenda kwenye madarasa, zahanati, hospitali, ujenzi wa jengo la utawala n.k, niwaombe watumishi wenzangu, tukazisimamie fedha hizi kikamilifu na kwa uaminifu mkubwa.”
amesema Sanga na kuongeza kuwa

“Tuache ‘wizi wa kisheria’ wa kufuata taratibu zote za manunuzi huku tukiwa tumezidisha bei ya vitu kwa maksudi ya kujinufaisha. Mimi kama Mbunge sitawaacha salama watumishi wote watakaohujumu fedha hizi ambazo Mh. Rais ameona vyema zije ziwasaidie wanamakete kwenye miradi yao ya maendeleo”.