Kamati za Kudumu za Bunge za Nishati na Madini pamoja na ile ya Bajeti zimewasili mkoani Mtwara kwa ajili ya ziara ya siku moja.
Kwa mkoa huo wa Mtwara, kamati hizo zinatembelea miundombinu ya kuchakata gesi asilia huko Madimba, visima vya gesi Mnazi Bay na miundombinu ya kupokea mafuta katika bandari ya Mtwara.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Nishati na Madini watatembelea miundombinu ya kuchakata gesi asilia Madimba na visima vya gesi Mnazi Bay.
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti yenyewe inatembelea miundombinu ya kupokea mafuta katika bandari ya Mtwara.
Baada ya ziara hiyo, kamati ya Nishati na Madini itatembelea mradi ujenzi wa bwawa la umeme la Julius Nyerere na kamati ya bajeti itatembelea mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).