Konde Music yaachana na Killy na Cheed

0
2221

Uongozi wa lebo ya Konde Music Wordwide umetangaza kuagana na kusitisha mikataba ya wasanii Ally Omary (Killy) na Rashid Manga (Cheed) kwa sababu mbalimbali zilizo nje ya uwezo wake.

Taarifa rasmi ya Konde Gang imeeleza kuwa wasanii hao kwa sasa wapo huru kufanya kazi na kuingia mkataba na kundi au mtu yeyote .

“Konde Music Worldwide haitahusika na jambo lolote litakalohusisha wasanii hawa kuanzia leo, tunapenda kuwashukuru Killy na Cheed kwa ushirikiano wao katika kipindi chote cha kuwa pamoja na tunawatakia mafaniko mema katika kazi zao hapo baadaye.” imeeleza taarifa ya
Konde Music Worldwide