Padri wa kanisa Katoliki Parokia Teule ya Mtakatifu Deonis Aropagita jimbo la Moshi mkoa wa Kilimanjaro, Sostenes Soka
leo amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi kusomewa maelezo ya awali katika tuhuma zinazomkabili za kudhalilisha watoto.
Septemba 26 mwaka huu Padri huyo alipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo na kusomewa mashtaka mawili, huku shtaka la tatu likifunguliwa katika mahakama ya wilaya ya Moshi.