Mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete, – Salma Kikwete akihutubia mkutano wa Wanawake Viongozi Barani Afrika unaondelea huko Bujumbura, Burundi.
Katika hotuba yake, Salma Kikwete amewaambia washiriki wa mkutano huo kuwa Tanzania imepiga hatua katika kupunguza vifo vya mama na mtoto kwa kuongeza idadi ya wakunga na madaktari bingwa katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Pamoja na mafanikio hayo, ameiomba serikali kuhakikisha vyuo vikuu vya afya vya Tanzania vinakuwa na vifaa vya kutosha vya kufundishia, ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya.