Yanga na Al Hilal hakuna mbabe

0
937

Yanga SC imelazimishwa sare ya 1-1 na Al Hilal Club ya nchini Sudan katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Yanga ndio ilikuwa ya kwanza kupata goli dakika 5 baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kupitia kwa Fiston Mayele, lakini dakia 17 baadaye, Al Hilal walisawazisha kupitia kwa Abdulrahman Yusuph.

Baada ya mchezo wa leo, timu hizo zitarudiana tena nchini Sudan Oktoba 16 mwaka huu ambapo timu itakayoshinda mchezo huo itatinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.

Yanga inakwenda na kaulimbiu, Iwe Jua, Iwe Mvua, kwamba lazima watafika hatua ya makundi.