Aua watu 38 na kujiua

0
225

Afisa wa zamani wa polisi nchini Thailand amewashambulia na kuwaua watu 38, wengi wao wakiwa watoto wadogo.

Habari kutoka nchini Thailand zinaeleza kuwa, afisa huyo wa zamani wa polisi amewashambulia watu hao akitumia bunduki na kisu.

Tukio hilo limetokea katika kituo kimoja cha kulea watoto katika mji wa Utthai Sawan.

Polisi nchini Thailand wamesema baada ya mtu huyo kufanya mauaji hayo, alikwenda nyumbani kwake na kuwaua mke wake na mtoto na kisha kujiua mwenyewe.

Mwezi June mwaka huu, mtu huyo aliyekuwa na umri wa miaka 34 alifukuzwa kazi baada ya kuthibitika anatumia dawa za kulevya.

Kati ya watu hao 38 waliouawa, 22 ni watoto wadogo.