Waziri Nape azindua bodi TBC

0
124

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ameiagiza Bodi mpya ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), kutunga sheria itakayoongoza shirika hilo katika utekelezaji wa majukumu yake kwa kubainisha vyanzo vya mapato.

Waziri Nape ametoa agizo hilo mkoani Dar es Salaam, wakati akizindua bodi hiyo.

Ameongeza kuwa utatuzi wa changamoto ndani ya TBC usifanyike kwa utashi pekee, bali kwa kuweka mifumo ya kudumu.

Bodi hiyo mpya ya TBC iliyozinduliwa leo inaongozwa na Mwenyekiti Stephen Kagaigai na ina wajumbe saba.