Samaki wawekewa minofu ya ziada kuongeza uzito

0
637

Wavuvi wa samaki katika mji wa
Cleveland nchini Marekani,
wamenaswa wakifanya udanganyifu kwenye uzito wa samaki.

Udanganyifu huo umefanyika wakati wa mashindano ya wavuvi yaliyoshirikisha wavuvi wa mji huo.

Maafisa wa uvuvi katika mji wa Cleveland wamedai kuwa, wakati wa mashindano hayo wavuvi waliongeza uzito wa samaki kwa kuwawekea vitu vyenye uzito pamoja na minofu ya ziada ndani ya samaki waliokuwa wakishindanishwa.

Samaki hao wanadaiwa kuongezewa uzito wa takribani kilo 3.6 kwa samaki wote watano waliopelekwa katika mashindano hayo ya wavuvi.

Mratibu wa mashindano hayo Jason Fischer amesema kuwa, samaki hao walionekana wadogo kuliko uzito waliokuwa nao, jambo lililosababisha wachunguzwe ili kubaini kama kuna udanganyifu wowote uliofanyika.

Kufuatia tukio tukio hilo Fischer ameonya kuwa, mvuvi yeyote anayebainika kubadilisha uzito halisi wa samaki wakati wa maonesho ya wavuvi ataondolewa mara moja kwenye mashindano.