Wasanii wa Tanzania waendelea kufanya Vizuri Kimataifa

0
1107

Wasanii wanne watanzania wanatarajia kushiriki katika msimu wa Coke Studio mwaka 2019 unaowashirikisha wasanii mbalimbali wenye vipaji barani Afrika na kuonyesha uwezo wao katika tasinia ya burudani.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa kitengo cha masoko Kenya na Tanzania Nelly Wainaina, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutangaza msimu wa Coke Studio kampeni ambayo itamwaga zawadi kwa watanzania ambao ni wapenzi wa burudani ya muziki.