Msimu wa kilimo Morogoro wazinduliwa

0
107

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Shaka Hamdu Shaka amezindua msimu wa kilimo katika mkoa wa Morogoro na kuwataka wananchi kutumia vema fursa mbalimbali zinazotengezwa na serikali ili kujiletea maendeleo.

Uzinduzi huo umefanyika katika kituo cha Utafiti wa Kilimo (TARI) Ilonga, wilayani Kilosa.

Shaka ametaja fursa hizo kuwa ni pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na kuanza kufanya kazi kwa treni ya mwendo wa haraka.

Ameongeza kuwa uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kuyatwaa na kuwapa wananchi mashamba 11 yaliyokuwa mikononi mwa wawekezaji ambao kwa muda mrefu wameshindwa kuyaendeleza, ni moja ya mambo makubwa ya kupigiwa mfano na kupongezwa yaliyofanywa na Rais.