Chanjale kujenga ofisi mpya

0
95

Wakazi wa kijiji cha Chanjale wilayani Mwanga mkoa wa Kilimanjaro wamejitolea nguvu zao kujenga ofisi mpya ya kijiji hicho baada ya kuona ofisi inayotumika hivi sasa ni chakavu na haifai kwa matumizi ya ofisi ya serikali .

Mwenyekiti wa kijiji hicho Salim Msofe amesema uamuzi wa kuvunjwa kwa banda la miti lililokuwa likitumiwa na kijiji hicho kama ofisi kwa kipindi Cha miaka 47 umefikiwa katika kikao kilichofanyika mwezi Januari mwaka huu kwa njia ya mtandao, ukishirikisha wakazi wote waliozaliwa katika kijiji hicho.

Amesema katika kikao hicho, wakazi hao walikubaliana kujenga ofisi mpya ya kijiji hicho, kama sehemu ya mchango wao wa kupeleka maendeleo kijijini walikozaliwa.

Hadi kukamilika kwake, ujenzi wa ofisi hiyo mpya ya kijiji cha Chanjale unatarajiwa kugharimu shilingi milioni 100.