Buchosa yatakiwa kuongeza ukusanyaji mapato

0
842

Mkuu wa wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, – Emmanuel Kipole ameiagiza Halmashauri ya Buchosa kuongeza  juhudi katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kupata fedha za kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo ile ya Elimu na Afya.

Kipole ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Buchosa.

Amesema kuwa  ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Shilingi Bilioni Mbili katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 pamoja na Shilingi Bilioni  Mbili Nukta Mbili katika mwaka  wa fedha wa 2019/2020 utawezesha kukamilishwa kwa miradi ambayo utekelezaji wake umekwama  kwa muda mrefu kutokana na ukosefu wa fedha.

Baraza  hilo  la madiwani la halmashauri ya Buchosa limepitisha mapendekezo ya bajeti ya Shilingi Bilioni 37 Nukta Saba katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 ikilinganishwa na bajeti ya Shilingi  Bilioni 36 katika mwaka huu wa fedha wa 2018/2019.