Azam yatakata mbele ya Singida BS

0
613

Azam FC imekwea hadi nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kuondoka na alama 3 katika mchezo dhidi a vijana wa Liti, Singida Big Stars uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa kuvutia uliokuwa na ushindani mkali, goli pekee na la ushindi limefungwa na Sospeter Bajana kunako dakika za lala salama katika kipindi cha kwanza.

Kwa kipigo hicho, Singida BS wanabaki kwenye nafasi ya 6 wakiwa na alama 8 kibindoni ikiwa na mchezo mmoja mkononi.