Rais awaapisha mawaziri aliowateua

0
151

Samia Suluhu Hassan leo amewaapisha mawaziri watatu kufuatia mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri aliyoyafanya hapo jana.

Mawaziri walioapishwa ni Angellah Kairuki ambaye ameapishwa kuwa waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wengine ni
Dkt. Stergomena Tax ambaye ameapishwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Innocent Bashungwa aliyeapishwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Mara baada ya mawaziri hao kuapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, walikula kiapo cha maadili.

Kabla ya mabadiliko hayo madogo ya baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais Samia, Dkt.Tax alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga na Taifa, na amechukua nafasi ya Balozi Liberata Mulamula.

Bashungwa yeye alikuwa Waziri wa TAMISEMI.