Bilioni 2.7 zatengwa kwenye utafiti Tiba Asili

0
226

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema Rais Samia Suluhu Hassan ana nia ya dhati ya kuwekeza kwenye tiba asili baada ya kutoa shilingi Bilioni 2.7 kwa ajili ya utafiti kwenye eneo la tiba Asili.

Dkt. Mollel amesema hayo alipokuwa akizindua kituo cha Tiba Asili cha Tiba Jumuishi cha Afrika Alama kilichopo kijiji cha Ngarenanyuki, Arumeru mkoani Arusha, kituo ambacho kinatumia mitishamba kutoa huduma za Tiba ya Afya.

“Nimekuja ili kuionyesha Tanzania Hospitali ya Tiba Asili, Rais wetu Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 2.7 kwa ajili ya utafiti kwenye eneo la Tiba Asili, Rais Samia ana nia ya dhati ya kuendeleza Tiba Asili. Tuwatumie hawa watu(Kituo cha Tiba Jumuishi cha Afrika Alama) kuwajengea uwezo watu wetu ili tuwe na Tiba Asili kama hii katika Hospitali zetu.”- amesema Dkt. Mollel

Dkt. Mollel ameongeza kuwa kuna majengo ya kutosha ya kutolea huduma katika hospitali ambayo yamejengwa na Rais Samia Sukuhu Hassan.