“Kwa upande wa mradi, tumeona hili bunge la Ulaya, halina taarifa za kutosha na limekuwa likitoa taarifa ambazo zinapotosha ulimwengu.
Kama wangelikuwa wanahitaji kujua taarifa za mradi walikuwa na uwezo wa kuja kuzungumza na Serikali ya Tanzania na Uganda ili wapate taarifa. Taarifa zimetoka nje ambazo sio za kweli,” amesema Abdulsamad Abdulrahim, Mdau na mwekezaji katika Sekta ya Mafuta