Wanaoisaidia Yemen matatani

0
1120

Bunge la seneti la Marekani limepitisha muswada unaozuia misaada kwa Mataifa ya Kiarabu yanayopigana kuisaidia serikali ya Yemen inayopambana  na wapiganaji wa kikundi cha Houthi cha nchini humo.

Marekani ilikuwa ikitoa misaada ya kijeshi kwa serikali ya Saudi Arabia ambayo imekuwa ikishirikiana na majeshi ya nchi wa shirika kupambana na wapiganaji hao wa kikundi cha Houthi nchini Yemen.

Hata hivyo katika siku za hivi karibuni wabunge kutoka Chama Cha Democrat walianza kuitilia mashaka serikali ya Saudi Arabia baada ya taarifa kueleza kuwa mwana wa mfalme wa nchi hiyo alihusika na kifo cha mwandishi wa habari na mwanaharakati Jamal Khashoggi.

Mwandishi huyo wa habari na wanaharakati aliyekuwa kiikosoa kwa wazi serikali ya Saudi Arabia aliuawa katika Ubalozi mdogo wa nchi hiyo ulioko mjini Istanbul nchini Uturuki mwaka 2018 na mwili wake haujapatikana hadi  sasa.

Wabunge wa Bunge la Seneti la Marekani pia wamekuwa wakiishutumu Saudi Arabia mara kadhaa kwa kufanya mashambulio dhidi ya raia nchini Yemen badala ya kuwalenga Wapiganaji.

Tukio baya zaidi lilikuwa la vikosi vya Saudi Arabia kushambulia basi la watoto waliokuwa wakienda shuleni na kuwaua.