Serikali imetoa shilingi bilioni 19 kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mtwara (MTUWASA), kwa ajili ya uboreshwaji wa mtandao wa miundombinu ya usambazaji maji mji wa Mtwara.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametoa taarifa hiyo mara baada ya kushuhudia utiaji saini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo kati ya MTUWASA na mkandarasi anayetarajiwa kutekeleza mradi huo.
Waziri Aweso ameagiza mamlaka husika kuhakikisha zinasimamia mradi huo ili utekelezwe kama ilivyopangwa na kuwanufaisha walengwa.
“Tusimamie mradi huu , moja ya changamoto ya miradi ya maji ni usimamizi ndugu zangu, hizi ni fedha zenu ,bilioni kumi na tisa zimeletwa kwa ajili ya kuwanufaisha, hivyo lazima tusimamie kwa dhati na kuleta matokeo.” ameagiza Waziri Aweso