Majaliwa ashiriki mazishi ya Shinzo Abe

0
327

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, leo ameungana na wakuu wa nchi na viongozi mbalimbali 700 kutoka nchi 195 duniani na wa mashirika ya kimataifa, kuweka mashada ya maua kwenye mazishi ya kitaifa ya Waziri Mkuu mstaafu wa Japan, Shinzo Abe.

Waziri Mkuu ambaye yuko Tokyo, Japan akimwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan, pia ametoa heshima za mwisho kwenye ukumbi wa Nippon Budokan, akiwa amefuatana na mke wake Mary Majaliwa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk,
Balozi wa Tanzania nchini Japan, Baraka Luvanda na mke wake Consolata Luvanda.

Baada ya kutoa heshima za mwisho, Waziri Mkuu Majaliwa alikwenda kwenye Kasri la Kifalme la Akasaka jijini Tokyo, ambako hufanyika shughuli zote za kiserikali ili kumfariji Waziri Mkuu wa nchi hiyo Fumio Kishida pamoja na mjane Shinzo Abe, Akie Abe.

Alikuwa miongoni mwa viongozi wengine wa kitaifa 40 waliopata fursa hiyo.