Balozi Mahmoud Thabit Kombo msibani

0
182

Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mahmoud Thabit Kombo
akisaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Paul Rupia nyumbani kwa marehemu Oysterbay mkoani Dar es Salaam.

Mazishi ya Balozi Paul aliyefariki dunia tarehe 16 mwezi huu nchini Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu, yatafanyika kesho katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.