Tanzania kuendeleza ushirikiano na Msumbiji

0
154

Tanzania imesema itaendeleza ushirikiano wake na Msumbiji uliodumu kwa muda mrefu kwa manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.

Kauli hiyo imetolewa nchini Msumbiji na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ameanza ziara yake ya kiserikali ya siku tatu nchini humo.

Rais Samia pia amesema katika mazungumzo na mwenyeji wake Rais Filipe Nyusi wamekubaliana kuimarisha ulinzi na usalama, maeneo ambayo wamekuwa wakishirikiana kwa miaka mingi.

Amesema kutokana na umuhimu wa ushirikiano katika eneo la ulinzi na usalama, ndio maana Tanzania na Msumbiji zimetiliana saini mikataba ya ushirikiano katika maeneo hayo mawili muhimu.

https://www.youtube.com/watch?v=Sitm_wGiQfE

Kuhusu uwekezaji na biashara, Rais Samia Suluhu Hassan amesema wamekubaliana kuendelea kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara na uwekezaji katika pande zote mbili ili kuwanufaisha wafanyabiashara na wawekezaji wa pande hizo.

Eneo jingine ambalo Rais Samia na mwenyeji wake Rais Nyusi wamekubalkana kushirikiana katika ufundishaji wa lugha ya Kiswahili katika taasisi za elimu nchini Msumbiji ili wananchi wa pande zote mbili waweze kutumia lugha moja.

Kwa upande wake Rais Filipe Nyusi amesema ili kupambana na vitendo vya kigaidi latika eneo la mpaka wa Tanzania na Msumbiji, ni lazima uwepo ushirikiano na ili kufanikisha ni lazima zifuatwe taratibu za kisheria kwa kuwepo kwa mikataba.