Watoto njiti Handeni wapata msaada

0
126

Taasisi ya kusaidia watoto njiti ya Doris Mollel kwa kushirikiana na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imesaidia watoto njiti katika katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga, kwa kutoa vifaa tiba kwa hospitali ya wilaya hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni 130.

Taasisi ya Doris Mollel imekua kinara katika kutoa vifaa tiba kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya watoto njiti kwenye maeneo mbalimbali nchini.