Leo ni siku ya Kimataifa ya amani, siku ambayo huadhimishwa Septemba 21 ya kila mwaka.
Siku hiyo ilianza kuadhimishwa mwaka 1981 baada ya kupitishwa na Umoja wa Mataifa.
Katika kuadhimisha siku hiyo ya Kimataifa ya amani, Umoja wa Mataifa umekuwa ukiwashauri wadau wa masuala ya amani pamoja na mataifa mbalimbali kusisitiza suala la amani na kuondoa mizozo katika maeneo yao.
Kitaifa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya amani yanafanyika mkoani Kilimanjaro, ambapo mgeni ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.