Vituo 1,859 kupima Kifua Kikuu

0
81

Serikali imepanga kuanzisha vituo 1,859 nchi nzima, kwa ajili ya kutoa huduma ya vipimo vya ugonjwa kifua kikuu ili kuwawezesha wananchi kupata huduma hizo katika maeneo yao.

Naibu waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameliambia Bunge kuwa, katika bajeti ya mwaka huu wizara ya Afya imepanga kuanzisha vituo hivyo ili kuwezesha upimaji wa ugonjwa wa Kifua Kikuu kupatika kwa haraka.

Dkt. Mollel ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mwantum Dau Haji, aliyetaka kujua ni nini mpango wa serikali katika kusogeza huduma ya upimaji wa ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa wananchi.

Dkt. Mollel ameongeza kuwa serikali pia inapeleka kipimo cha Xray za kidijitali, ambazo zitakua zikitembea na hivyo kuwawezesha watoa huduma kuwafuata wananchi katika maeneo yao na kutoa huduma ya vipimo katika maeneo yao.