Media day 2022

0
71

Mkurugenzi wa Huduma za Redio kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Aisha Dachi (mwenye nguo ya njano), ni mmoja wa waliokuwa waongoza mjadala wakati wa semina kwa waandishi wa habari kuhusu habari za biashara na uchumi.

Semina hiyo iliyoandaliwa na benki ya CRDB imefanyika mkoani Dar es Salaam.

Wengine walioongoza mjadala huo ni Bakari Machumu ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd na Dkt. Darius Mukiza ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wakati wa semina hiyo benki ya CRDB iliweka wazi mpango wake wa kuendelea kufadhili masuala ya utafiti unaohusu uchumi, fedha na biashara kwa waandishi wa habari wa hapa nchini.