Mpango kabambe sekta ya Uvuvi wa zinduliwa

0
198

Wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa mpango kabambe wa sekta ya uvuvi ambao utatekelezwa kwa kipindi cha miaka 15 kuanzia 2021/2022 hadi 2036/2037, uzinduzi uliofanywa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mkoani Dar es Salaam.

Miongoni mwa wageni hao ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mahmoud Thabit Kombo (wa nyuma ya Waziri Mkuu kushoto), ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo ( IFAD) ambapo mashirika hayo yote Makao Makuu yake yapo nchini Italia.